Karibuni katika blog ambayo itakuwa inaelezea mambo ya kinajimu (astrology), mawe ya bahati ya kinyota, matukio kinyota na kiutabiri, matukio kimataifa na kimataifa na wanaopenda kujifunza elimu hii, mafusho,kuongelea viumbe kama majini, malaika, mizimu, freemason na iluminat, tiba kwa njia ya vyakula na matunda, magonjwa kinajimu na tiba zake.

Wednesday, November 30, 2011

Watu wenye asili ya upepo na tabia zao

Watu wenye asili ya Upepo na tabia zao May 21- June 20 na September 23 - October 22 na January 20 - February 18, na watu wenye kuanziwa na herufi C, O, S,G, K, W au watu waliozaliwa tarehe 3, 7, 11, 15, 19, 23,27 na 31 au watu wenye sauti nzuri, wenye athari katika vifua vyao au migongo yao, watu wafupi wenye miguu minene,wenye kunyoa vipara au watu wenye rangi ya kuteleteza na wenye mikono myepesi au watu wenye vifua vya kutanuka, wenye mdomo ulio kolea weusi na pua yenye ubapa wenye macho ya kati kwa kati watu hawa tabia zao ni watu wanaopenda kusaidia watu, wanapenda kushauri wenzao pasipo wao kushauriwa na ni watu wenye kupata umaarufu na ni watu wenye kupenda kujishughulisha kibiashara na ni watu wenye kupenda kuwasaidia hata maadui zao pasina kujali ni wenye kubadilika badilika na wenye uamuzi wa haraka ni watu wenye kupendwa na watu kwani kazi wanazozifanya ni kazi kushawishi watu au za kuburudisha watu na pia hutegemewa na watu katika kazi zao na wana bahati ya kupendwa na wazazi wao na watu wenye kupenda kujipumzisha kwenye upepo na kipato chao ni chenye kubadilika badilika na ni watu wenye kupenda kusaidiwa na watu fulani na watu hawa mara nyingi huwa hawakai na mpenzi zaidi ya mmoja na hupendwa na wapenzi wasio wapenda wao, Kazi zao hutegemea majira na mara nyingi watu hawa hujishughulisha na shughuli za kuwaburudisha watu, wanapendeza kutoa hutuba na kujishughulisha na siasa na uamuzi wao wa haraka japo hubadilika badilika na ni watu wanaopatwa msongo wa mawazo na mapigo ya moyo kwenda kasi na huwa wnkazi ya ziada kuwaweka sawa wapenzi wao kwani wapenzi wao huhitaji ushauri kutoka kwao wakati mwingine watu hawa huwa ni watu wenye maringo, hupendelea mapambopambo,kujiajiri wao na hupata umaarufu kwa njia wasizozitegemea wao, na huwa na bahati ya kupata marafiki wengi wake kwa waume wakubwa kwa wadogo kutokana na tabia yao ya uaminifu na ukweli na watu hawa maadui zao wengi ni wenye nyota ya udongo kwani watu wa udongo hawapendi kusifia wenzao na hawa wanapenda kusifiwa na mungu huwajalia huishi maisha marefu.
Kazi za watu wa asili hii ni wanamziki,watangazaji,ufundi wa vyombo vya umeme, falsafa, uandishi,siasa, utumishi, kazi za serikali na hujishughulisha na biashara zao ambazo huwaletea matatizo, watu hawa wanabahati ya kukutana na wapenzi wenye asili ya moto na wapenzi wao hunyanyuka kwa kupitia wao, watu rangi zao za kinyota ni kijani kibichi, bluu bahari, kijivu,rangi ya fedha, njano watu hao wanashauriwa kutumia vyakula vyenye utamu utamu mfano matunda yenye asili ya unjano na utamu na wanashauriwa kutumia manukato yenye harufu nzuri wanashauriwa watu hawa kwani hukutana na watu mbalimbali na elimu yao huwasaidia kufika mbali. na nyota zao ni mapacha, mizani, ndoo.
Madini yao ni fedha, shaba, aluminium na mawe yao yawena asili ya ukijani, njano au rangi za kuvutia kwani nyota zao ni za kuvutia vile vile watu wa nyota hii wanashauriwa sana wakae sehemu za mwinuko au sehemu zenye uwanja mkubwa au pembezoni mwa mji watumie hizi kustarehe na wapenzi wao kwani wapenzi wao wa majanga utafutaji wa pesa unahitaji akili nyingi na utunzaji japo ni watu wa kutoa toa pesa hovyo. Mafusho ya nyota zao ni kachiri, mushtaka na miatusaila kwa watu wenye nyota ya ndoo na siku zao ni jumatano kwa mapacha, Jumamosi kwa ndoo na ijumaa kwa mizani kinyota watu hawa wanashauriwa kuwaunganisha marafiki kimapenzi kwani nyota zao ni nyota za kukusanya watu, wanashauriwa kuvaa nguo zenye kupendezesha na kwenda na wakati na mavazi yao mara nyingi yawe ni rangi moja na wanawake wao wanashauriwa kuvaa mapambo sana na viatu virefu, na wanawake wao wanashauriwa kutunza nywele japo hawapendi na mikoba wapende kuvaa. wanashauriwa watembe kwa mwendo wa madaha kwani huwafurahisha wapenzi wao na wapende kuwasemea sauti za chini na kuwaliwaza wawashike wapenzi wao vichwa,shingo zao na masikio yao na wawaminye minye mikono yao watawafurahisha wapenzi wao na washughulike sana wanapokuwa faraghani na wapenzi wao wawashe redio kwa sauti ya chini, muziki wa taratibu au nyimbo zenye kusikitisha na kuonewa, wawashe feni kidogo pembeni, na kwenye falagha wawasifie wapenzi wao kwani huwafurahisha na kuwapa chochote wanachotaka watu hawa  hupendwa na ndugu wa wapenzi wao.
Watu wenye asili hii kwa mwaka huu.
Watu wenye asili hii kwa mwaka huu maisha yao yamekuwa kawaida japo wamepoteza wapenzi wao waliowapenda sana na mwaka huu watu wa nyota hii wameanza kutafuta mali au jambo jipya japo linasuasua na mwaka huu wameandamwa na maradhi ya kutokujiamini na akili zao kufumba, na wamekutana na wapinzani wao katika shughuli zao wanashauriwa wakae na watu hao wasiowapenda kwani sasa hivi wanamatatizo wanahitaji msaada wa kifedha, kimali na kielimu kwani hao watu wasiowapenda ndio wanamsaada wao japo wa muda na sasa hivi watu hawa wanapenda kukaa kwenye makundi pasina maendeleo yoyote kuwashauri wenzao japo wenyewe wanamatatizo na mwaka huu wamepoteza kazi walizokuwa wanazitegemea na fani zao walizokuwa wanazitegemea zimeingia uzito kidogo, wawe makini kwani watu wanawaandalia kashfa ya uzinzi, pia watu hawa sasa hivi wanasumbuliwa na upepo wa ummu subiani ndio maana wakiamkaa huwa wanachoka na kutetemeka katika usingizi wao na kujihisi wavivu na ndoto mbaya, na hujihisi kuna kitu katika mgongo wake au kifua chake na huandamwa na hali za unyonge katika nafsi zao, wanashauriwa wawaone wazee wao wa dini wawafanyie dawa au maombi na kuondolewa upepo huo wa ummu subiani inshallah mungu atawasaidia.
Watu wenye asili hii kwa mwaka 2012.
Watu wenye asili hii ya upepo kwa mwaka huu utakuwa ni wenye faraja kwani kiu ya mambo yao yatakuwa na dalili ya kupatikana na maswala yao yaliyo kwama yatafunguka na wanauwezekano mkubwa wa kupata wapenzi wapya na wanashauriwa wawe makini katika maswala yao, wanashauriwa washirikiane na watu wenye asili ya moto au kiongozi fulani mkubwa wa kisiasa, kitamaduni na muda wao mzuri wa kujipanga katika elimu na mwaka wao mzuri wa kuanzisha mambo ya kisanaa watafanikiwa, wanashauriwa wasiende nchi za magharibi au magharibi kwani hawatofanikiwa jambo lao lolote. kimsingi watoe sadaka sana na wagawe vitu sana na wajitahidi kutafuta utatuzi wao wa uzazi na ni muda wao mzuri kuanza maisha yao mapya ya kifamilia au kindoa  hii ni kwa ufupi tu.
Nchi zenye asili ya upepo zitatawaliwa na jua na mvua zenye upepo mkali na wawe makini kwani kinaweza kutokea kimbunga chenye kuambatana na maji na nchi hizi zitashirikiana na nchi zenye maahasimu wao na zitapatikana suluhu katika migogoro yao na raisi na viongozi wengi watapatikana kwa njia ya halali kwani inaelekea kutakuwa na chaguzi nyingi katika nchi hizi na watatembelewa na viongozi wakubwa katika nchi kubwa na kutasikika habari ya wanamuziki, kuungana, kuoana katika dunia au kupata mali kwa msanii na watu wengi watapata ufahamu na kutagundulika baadhi ya siri zilizofichika kisiasa ili nchi hizi ziishi kwa amani na vyakula vya matunda vitakuwa vingi na nchi hizi zinashauriwa kujenga ujamaa na utulivu hii ni kwa kifupi tu.

7 comments:

  1. nimezaliwa may 25 mwezi wa tano jina linaanza na d nimesomea utangazaji nyota yangu ni ipi na ina asili gani namambo yake

    ReplyDelete
  2. Mimi nimezaliwa 20 August mafusho yangu ni yapi?

    ReplyDelete
  3. Na nyota yangu ni hipi jina langu limeanza na P

    ReplyDelete
  4. kwanini wati hawa wenye asili ya udongo wanashuriwa wasisafiri kuna shida gani?

    ReplyDelete
  5. asili ya upepo samahani na si udongo

    ReplyDelete
  6. Nitumie utabiri wa mwaka huu 2019

    ReplyDelete
  7. Naomba utabiri Wa Nyota ya ndoo 2019

    ReplyDelete