Karibuni katika blog ambayo itakuwa inaelezea mambo ya kinajimu (astrology), mawe ya bahati ya kinyota, matukio kinyota na kiutabiri, matukio kimataifa na kimataifa na wanaopenda kujifunza elimu hii, mafusho,kuongelea viumbe kama majini, malaika, mizimu, freemason na iluminat, tiba kwa njia ya vyakula na matunda, magonjwa kinajimu na tiba zake.

Wednesday, December 7, 2011

Watu wenye asili ya udongo na tabia zao

Watu wenye asili ya udongo na tabia zao  April 20 - May 20, Augost 23 - September 22, December 22 - January 19, na Majina yanayoanziwa na herufi B, N, Z, F, R, J, V, au waliozaliwa tarehe 1, 6, 10, 14, 18, 22, 26, 30 au watu wenye mikono yenye nguvu, maumbile makubwa ya kimwili watu wenye miraba minne na wenye rangi ya kuteleza na wenye mikono na miguu bapa, na watu wenye rangi ya chocolate au wekundu wa chocolate. watu wa asili hii wanatabia ya utulivu pasina papara na utaratibu pasi na haraka, wapole mbele ya macho ya watu na wenye tabia ngumu kiusiri, watu hawa hawaonyeshi uasilia wao mbele ya macho ya watu, watu hawa wakiwa wanaume sio waongeaji sana tofauti na wanawake wa asili hii, mara nyingi wanawake wa asili hii huongea kwa kudeka, watu wenye asili hii hupenda kujifanya wanaelimu au matajiri hata kama hawana elimu wala utajiri na wanapenda marafiki wenye pesa, watu hawa mara nyingi wanafanya kazi ngumu na nzito na wanapenda kujitegemea pia watu hawa wanabahati mbaya ya kuachwa upweke na familia zao au kufiwa na wazazi wao, watu hawa hupendwa na wazazi wa kike, watu hawa hupenda ufuska wa chini chini na huwa hawajali lolote  wanapopenda, wanatabia ya kuugua ugua mara kwa mara na wakati mwingine hupenda kubadilisha dini zao au makabila yao au mila zao, watu hawa huwa wazembe wanapopenda ila mungu aliwajalia kuwa watu wenye nguvu katika maisha, hupenda kufikiri jambo kabla hawajaliamua hata kama uamuzi wao sio sahihi, watu hawa hawapendi ubishani hata wakijua unakosea wanakuacha na ujinga wako. Watu hawa hufanya kazi pasipo maneno mengi wanabahati mbaya ya kupata wapenzi mapepe na waongeaji hovyo, katika maisha yao watu hawa hukumbwa na mitihani mingi sana pasipo msaada wa ndugu au mtu yeyote hii huwafanya kujenga chuki na ndugu zao na kuamua kuishi peke yao pia watu hawa hupenda kujitegemea wao pasipo kutegemea, watu hawa huwa hawadumu na mpenzi mmoja ila mara nyingi huwapenda wapenzi wao wa mwanzo au waliowasaidia japo hupata nao migogoro mingi, hukumbwa na kashfa katika maisha yao za ubakaji, ulevi, uzinzi, wizi, ubakwaji hii huwa haribu sana kisaikolojia, watu hawa hupenda kufanya mambo yao kisiri siri na huwa sio wakweli na huwa hawakatai mapenzi wanapo tongozwa na ni watu wanao kaa na ashki sana pasipo kuonyesha, watu hawa hupenda kuingiliwa kimaamuzi na watu wenyine kwani huonekana ni wazembe hawana fikra zozote, pia wana bahati ya kung'ang'ania penzi lisilokuwa na ukweli na pesa zao nyingi huwa ni za msimu na watu hawa hupenda kusema na nafsi zao pasipo kuwaambia watu wengine na hawapendi kupaparikia mambo hata kama wanayapenda, watu hawa huwa na mitihani mingi sana lakini wanapata bahati sana na watu hawa hawaoni hatari kugombana na wazazi wao kwaajiri ya wapenzi wao na pia watu hawa huwa wavumilivu sana wakati wa shida, Watu hawa hawapendi vurugu na wanapochokozwa wana nguvu na mabavu sana pia watu hawa wana maamuzi yao pasipo kushirikisha watu wengine, Kazi zao nyingi huwa za asili ya upepo, wana kazi nyingi za mkono kama uchoraji, uandishi, upiganaji, uanajeshi, uchezaji wa mpira na michezo kwa ujumla na hupenda kazi za ofisini na wanabahati ya kupata kazi hata kama hawana elimu,watu hawa hujikuta wanfanya kazi hata kama hawana hobi nazo, pia watu hawa hawaamini maswala ya uchawi, dini zao, mila zao mpaka yanapowakuta matatizo na watu hawa hupenda kutumia dawa sana wanapokutwa na maradhi, na watu hawa kimapenzi wana nguvu za ajabu na huwa hawapendi kujisifia huonyesha matendo katika mapenzi, hupenda kuchezeana chezeana na wapenzi wao,
Madini yao ni shaba,petrol, ngozi, au vitu vinavyooshwa na petroli, madini ya risasi na fedha na rangi zao za kinyota ni nyeupe, kijani kibichi, udhurungi, nyeusi kwa watu wa nyota ya mbuzi, mafusho yao ni mushtaka, kachiri, miatisaila, siku zao ni ijumaa, jumatano na jumamosi maradhi yao ni mgongo, misuri, miguu kwenye vifundo, kifua, tumbo kujaa gesi, figo au ini, na nyota zao ni ng'ombe, mbuzi, mashuke na maadui zao ni watu wenye asili ya moto na upepo na wapenzi wao ni wenye asili ya maji na hayo ni kwa ufupi tu.
Watu wenye asili hii kwa mwaka huu.
Wamejikuta wakishughulika na mambo mengi ya kimaisha na mwaka huu umekuwa hauna heri wala shari japo wengine wamefukuzwa kazi au wameachwa na wapenzi wao, na mwishoni mwa mwaka huu wamejikuta kwenye matatizo na malumbano ya kifamilia au kikazi kwani baadhi ya watu wao wengine humpenda wangine hawampendi hujikuta wanaingilia penzi au wameingiliwa penzi na watu wakaribu yao ila akili zao zinawatuma kutafuta maisha pasipo kujali ndani ya nafsi zao .Sasa hivi nafsi zao zinasema hatama ya maisha yoa na hapo wanatafuta jambo wanahisi wakilipata wanahisi watapata nafuu ya maisha kwani wanaahidiwa mambo mengi na jamaa zao, kwa mwaka huu wamepata habari za harusi za ndugu zao au jamaa zao pia wanafikiria kuhusu watu aliopotezana nao miaka miwili mpaka minane iliyopita watu hawa wamepotezana nao au wamefariki, au wamefilisika kwani watu hawa walikuwa wakiwapa msaada,  Watu hawa wanabahati ya kuwa watu wazuri wanashauriwa kwa mwaka huu kuwa makini kwani ndipo faraja huja.
Watu wenye asili hii kwa mwaka 2012.
Wanajikuta bado wanatafuta  msaada kwa ajili ya matatizo yao lakini nawatabiria watakua ndani ya mitihani miziti bado na watashirikishwa kwenye mambo yasiyo wahusu, na wataendelea kupata taarifa za harusi pia watafiwa na rafiki au jamaa wa karibu au bosi au mfanyakazi mwenzao na mwaka huu ukifika katikati watapata nafuu ya maisha yao ila wawe makini kwani watapata maradhi ya miguu, wenye ndoa zao waendelee kuwa na ndoa zao wasiziache pia wanawake wa nyota hii wawe makini kwani wapenzi wao wanataka kuongeza, wake wengine, wanashauriwa kuwaona wataalamu wa kinyota kuwatengeneza au wakidini ili kuwaombea kuwaweka sawa kinyota pia kuna uwezekano watu wa asili hii kukutana na wapenzi wapya japo kutakuwa na kelele kutoka upande mwingine.
Nchi zenye asili hii kwa mwaka huu, ni nchi kubwa zitajikuta zikiwa bado katika vita na barozi zao kushambuliwa zaidi na watajikuta katika malumbano ya kisiasa na wananchi wao baadhi ya nchi hizi zitakumbwa na ukame, na nchi hizi zitatoa tamko la kugundulika dawa au tutatua matatizo ya kijamii na kuna kiongozi mkubwa katika nchi au serikali kufariki kwa ajali au maradhi ya muda mrefu na uwezekano wa mwanamziki au mtu maarufu kufa na habari hizo zatazagaa mashariki na magharibi na nchi hizi zitapata majibizano na nchi za mashariki na kuna kiongozi wa nchi kubwa atapata maradhi au kufa na ni wakati mzuri kwa nchi hizi kusaidia nchi zilizo chini yao kwani zitawafanya wapate nguvu zaidi kuna uwezekano mkubwa wa chombo cha usafiri kupotea au kuanguka au kuzama sehemu yenye maporomoko au milima mikubwa, na nchi hizi zitaweza kuzuia mashambulizi makubwa katika nchi zao.

No comments:

Post a Comment