Karibuni katika blog ambayo itakuwa inaelezea mambo ya kinajimu (astrology), mawe ya bahati ya kinyota, matukio kinyota na kiutabiri, matukio kimataifa na kimataifa na wanaopenda kujifunza elimu hii, mafusho,kuongelea viumbe kama majini, malaika, mizimu, freemason na iluminat, tiba kwa njia ya vyakula na matunda, magonjwa kinajimu na tiba zake.

Saturday, December 3, 2011

Watu wenye asili ya maji na tabia zao

Watu wenye asili ya maji na tabia zao June 21 - July 22, October 23 - November 21, February 19 - March 20, Majina yanayo anziwa na herufi D, P, H, T, L, X, na watu waliozaliwa tarehe 4, 8, 16, 12, 20, 24, 28 au wenye shepu zifuatazo, shepu za duara au za mraba, pua ya duara au watu wenye matatizo ya tumbo, watu hawa ni watu wenye akili sana na ni watu wenye kusoma sana, kutunza na kuhifadhi mambo kwa muda mrefu wenye kupenda kukaa na mizigo, ni watu wenye kupenda mashindano, wenye vigeugeu sana,wenye kulaumu laumu sana na ni watu wenye hisia na kuhisi kitu kikawa wawe makini na watu hawa kwani watu hawa wakikusemea jambo huwa, Watu hawa huanza bahati ya kupendwa na watu utotoni na mabibi zao, shangazi zao, wajomba zao, wazazi wao na watu hawa hujihisi ni wenye bahati sana na wazazi wao huhisi kuwa watu wa asili hii watakuwa wanategemewa kwasababu ya bahati zao za utotoni, wanapofikia baleghe huanza kukutwa na matatizo lakini ni watu wenye sifa ya kuwa na elimu katika familia zao watu hawa pia hugeukwa na watu wanao wategemea na pia huwa wana ugomvi na ndugu zao hasa wakike na  pia hulaumiwa kwa ugomvi kwani ni watu wenye kelele, watu hawa pia wana tabia ya kuto kuwapenda watu wenye kimbelembele, hupenda kuingilia kazi za watu kwani hujiamini wanaweza kufanya shughuli hizo na watu wenye kuchemsha akili sana kwenye shughuli zao pia watu hawa tabia zao ni zenye kubadilika badilika kutokana na watu wanaokutana nao, wanapenda kuwaamrisha wenzao na wanapenda kuwamiliki ndugu zao hasa wakike wanaofuatana nao na hilo huwaletea matatizo na ndugu zao hao.  Hawa hujifanya au huonekana na elimu hatakama hawana elimu, watu hawa ni waongeaji pindi unapo wazoea pia watu hawa ni wakali kwenye pesa na hujifanya hawana pesa hata kama wanazo huwa wanatabia ya kushindana na wapenzi wao, pia wanabahati ya kupendwa na wapenzi wenye pesa lakini hujikuta wanaangukia kwa wapenzi mafukara na mara nyingi maradhi yao mengi ni ya tumbo na moyo kupiga na pesha kushuka wanapopata matatizo au habari mbaya na pia wanabahati ya kusikilizwa na mzazi wa kike na hii huwakera ndugu zao na wanabahati ya kupendwa na mabosi wao wakubwa na hii huwakera wafanyakazi wenzao, watu hawa hupewa sifa ya ufitinishaji, utapeli, uongo na ni watu wenye makusudi makusudi na wanaume wenye nyota hii huonekana mazoba na matapeli japo huonekana tofauti na wanawake wa nyota hii. Wanapenda kusimamia shughuli za kifamilia na mwisho wa shughuli hizo hawapati sifa ila lawama.
Wanawake wa nyota hii huwa watafutaji na washindani wa kimali na watu wenye asili ya moto na watu hawa huwa na wasiwasi wa kuibiwa pia huwa ni wepesi wa kulia wanapo jitetea na watu hawa huwa na nguvu ya kushinda kesi hata kama wao wamekosa wanashauriwa kukaa na wapenzi wenye kumcha mungu kwani hii huwasaidia kukaa sawa, wanawake wanabahati ya kuolewa na wanaume weusi au wenye sura mbaya au wasiokuwa na mvuto, ni watu wenye kuakaa na kazi zao wenyewe kwa muda mrefu kwani wapenzi wao ni wenye nyota ya udongo na hukumbana na matatizo wanapofunga ndoa kuanzia siku mbili, wiki mbili, miezi miwili, miaka miwili na pia wanaume wa asili hii wanabahati ya kuoa wanawake wanowazidi umri, weusi au wenye sura isiyokuwa na mvuto na wanawake huwa ni wataratibu sana watu wa asili hii hupenda kufanya mapenzi kwa muda mrefu ndio maana huwa penda watu wenye asili ya udongo kwani mambo yao ni taratibu na wanaweza kuwahimili watu wa maji, wanashauriwa waoge kabla ya kukutana na wenza wao na wanatakiwa wao wawaanze wapenzi wao kwani wapenzi wao ni watu wa taratibu na wazito wazito na watu hawa wanashauriwa wapunguze lawama kwa wapenzi wao. wanashauriwa wawachezee wapenzi wao sehemu za shingo,tumboni, mapajani, wataniane na wapenzi wao na wanapotaniwa na wapenzi wao huwa ni wenye kusitasita na kukataa na mapenzi yao mara nyingi wayafanyie pembezoni mwa kitanda au kwenye kochi au kiti na wapende kutandika mavazi makubwa ya rangi ya nyota zao wawaeleze shida zao wapenzi wao baada ya kukutana nao na hii ni kwa ufupi tu. Kazi za watu hawa ni uhaziri, uhasibu,uuguzi, utumishi wa umma, ualimu biashara ya vyakula na masoko na biashara za kuhudumia watu kwa ujumla.
Madini yao ni madini ya fedha, aluminium na chuma na rangi zao ni nyeupe na nyekundu kwa watu wa nyota ya nge na nyota zao ni kaa, ngee na samaki wanashauriwa kula vyakula vyenye asili ya weupe na matunda yasiyokuwa na radha na vitu vyenye maji mengi, mafusho yao ni ubani maka, udi kafru, sandari ahmari na namba zao nzuri za bahati ni 4, 8 na 12,  siku zao ni jumatatu,jumanne na alhamis na mawe yao ya bahati yana asili ya weupe na damu ya mzee.
Watu wenye asili hii kwa mwaka huu.
Watu wenye asili hii kwa mwaka huu wamekutana na matatizo mengi ya kuchukuliwa wapenzi wao na ndoa zao kuingia matatizo na kugombana na baadhi ya ndugu na shughuli zao kuwa katika hali ya kati na kati na sasa wanawapenzi wa nnje kama kisasi kwa wapenzi wao na wapenzi ambao wako mji mwingine au upande mwengine na hao wapenzi wao wanawake wengine au familia nyingine, mwaka huu wamesherekea harusi za ndugu zao wakaribu na watu hawa wameenda miji mingine au sehemu zingine kutafuta msaada wa kitiba kwani mwaka huu wameandamwa na maradhi ya tumbo na miguu na hivi sasa wanampango wa kuishi kipeke yao peke yao na familia zao kwani wanajihisi ni wenye mikosi na kuonewa na mwaka huu wamejikuta wakipata habari za mapenzi sana yawe ya shari au ya heri na baadhi ya shughuli zao walizisimamisha kwa muda ila muda si mrefu watapata kazi katika sehemu zenye kuhudumia hudumia au biashara hii ni kwa ufupi tu
Watu wenye asili hii 2012.
Bado watakuwa kwenye mitihani kwa kipindi kifupi, ila maradhi yao yatakuwa katika hali ya kuondoka wanashauriwa watafute watu wa kuwasaidia, kwa mwaka unaokuja watapata utatuzi au watoto, mali au kazi mpya na wapenzi wao kuomba kurudiana nao na ndio mwaka wa kutoa tamko lao ila wawe makini kwani wanaweza kuhamishwa sehemu za kazi zao au kulipwa mafao yao au kuhama majumba wanayoishi na wanashauriwa kukaa na watu wenye asili ya moto kwani watu wamoto ndio mwaka wao wa kutawala, wajihadhali sana kujibu majibu ya dharau kwani ni wakati wa maadui zao kujipanga, mwaka huu watakutana na watu maarufu au kupata msiba mkubwa wa kifamilia hasa mwenye asili ya kike au mwanaume wenye umaarufu katika familia na zitasikika habari za uongo kuhusu wao wanatakiwa wajipange na wao pia ila kwa siri pasipo kusema na mwaka mzuri wa kutafuta pesa na watafanikiwa na wapenzi wao watapata matatizo ya kifedha, na watu hawa watapata elimu au kutembelewa na watu wajuzi.
Nchi zenye asili ya maji zitakumbana na lawama au maneno na yataendelea kukataliwa  mambo yao wanayoyafanya na nchi zingine watajikuta kwenye malumbano ya kisiasa katika nchi yao na baadhi ya viongozi wao kutaka kujiuzulu au kujiuzulu na baada ya matatizo hayo itakuwa faraja kwao na watapata msiba wa kiongozi wao mkubwa mwenye matatizo ya miguu na moyo au mwanamke mkubwa katika serikali na vifo hivi si kwa nchi hizi tu ila kwa ulimwengu mzima na litatokea tamko kubwa katika nchi hizi litakalo washangaza watu na kuwasikitisha au kuwafurahisha jambo hili litasababisha maandamano na marumbano na mikusanyiko ya watu na hii ni kwa ufupi tu.

1 comment:

  1. Casino - Dr. Maryland
    The most important thing to 통영 출장마사지 do when 구리 출장안마 you gamble in the casino 경주 출장안마 is to ensure the players are dealt the The best place 상주 출장샵 to do this is at 오산 출장마사지 a casino with no

    ReplyDelete