Karibuni katika blog ambayo itakuwa inaelezea mambo ya kinajimu (astrology), mawe ya bahati ya kinyota, matukio kinyota na kiutabiri, matukio kimataifa na kimataifa na wanaopenda kujifunza elimu hii, mafusho,kuongelea viumbe kama majini, malaika, mizimu, freemason na iluminat, tiba kwa njia ya vyakula na matunda, magonjwa kinajimu na tiba zake.

Monday, November 28, 2011

Maana ya Astrology (Elimu ya Unajimu)

Astrology (Elimu ya Unajimu) ni elimu inayohusiana na mwenendo na tabia za viumbe hai na nyota pamoja na anga. Elimu hii ni elimu inayotaka kuhusiana au kuendana na elimu astronomy ila utofauti wake ni kuwa astrology inaelezea sana mwenendo wa viumbe hai kwa ujumla na inahusisha viumbe hai na anga, ila elimu ya astronomy inaelezea elimu ya anga peke yake.

Kwa maana hiyo manajimu wanaamini elimu ya anga ambayo ni nyota,sayari na mwezi zina uhusiano wa kitabia,kiasili, kimaumbile,kimaisha ,kimali,kimaradhi,kitiba na kifo na kimajira ya sayari ya dunia na vilivyomo.
Astrology ni neno la kigiriki lenye maneno mawili yaliyo ungana yenye maana, astro ni anga na logy ni viumbe hai.

Nini Asili yake?
Baadhi ya dini na makabila wanahusisha elimu hii na utawala wa miungu yao au mizimu yao kiujumla zote hizo ni imani tu kwa jinsi wanavyoamini wao.
Elimu hii ina uhusiano na uumbaji wa mwenyezi mungu mmoja ambaye ni yehova, allah (s.w), aliumba kila kitu kwa mahesabu kwa hiyo mahesabu haya yalitumiwa na mwenyezi mungu. Wanajimu wanaamini hesabu hizi zina uhusiano na elimu ya unajimu.

Je ina uhusiano gani na mienendo ua kishetani?
Watu wengine wanaamini elimu hii ni mienendo ya kishetani kitu ambacho si kweli, elimu hii haihusiani na kishetani ila baadhi ya mila, makabila fulani za watu fulani zikiwepo za kidini na za kikabila huipelekea hii kwenye maswala ya kishetani.

Mahusiano katika uumbaji wa mungu.
Jehova ambaye ni mungu aliumba vitu hivyo kutoka  katika asili yake yeye, asili ya kila kitu ni moja ambayo ni yeye mwenyewe. Yehova aliumba vitu vinne ambavyo ammbavyo vitu hivyo vikatoa asili ya vitu vyote katika ulimwengu ambayo ni
Moto ambao aliuweka upande wa mashariki, Upepo ambao aliuweka upande wa kaskazini, Udongo ambao aliuweka upande wa  magharibi na maji ambayo aliyaweka upande wa kusini.

Uumbaji huuu ni kwa mujibu wa elimu ya unajimu kwa hiyo kila kitu katika ulimwengu huu wakiwepo malaika, majini, binadamu, wanyama, mimea, bahari, anga, ardhi, mbingu, jua, mwezi vyote vinatokana na hii asili nne.
Asili hizi nne ziliweza kuzaa asili saba na matawi yake mawili ambayo mungu aliumba mbingu saba, ardhi saba, bahari saba, mabara saba, sayari kubwa zipo saba, kwa hiyo inaaminika vitu hivyo saba vinatokana na  asili hizo nne.

No comments:

Post a Comment