Karibuni katika blog ambayo itakuwa inaelezea mambo ya kinajimu (astrology), mawe ya bahati ya kinyota, matukio kinyota na kiutabiri, matukio kimataifa na kimataifa na wanaopenda kujifunza elimu hii, mafusho,kuongelea viumbe kama majini, malaika, mizimu, freemason na iluminat, tiba kwa njia ya vyakula na matunda, magonjwa kinajimu na tiba zake.

Tuesday, November 29, 2011

Watu wenye asili ya moto na tabia zao

 Watu wenye asili ya moto na tabia zao Machi 21- April 19 na July 23- Augost 22 na November 22- December 21 na watu wanao anzia na herufi zifuatazo A, M, Y, E, Q,I, U. Hawa watu wana asili ya moto na kimaumbile ni watu wenye uso mwembamba, pua yenye kuchongoka, wenye vidole virefu vya mikono, na vidole virefu vya miguu, watu hawa wanatabia ya mambo ya haraka haraka, ni watu wenye hisia kali na wenye mipango mingi ya kitamaa na wenye kutumia akili zao katika utafutaji na watu wenye kupenda kuwazidi wenzao katika kifamilia na kikazi na ni watu wenye mbinu nyingi katika utafutaji wao hawaoni hasara kuharibu jambo alimradi watimize lao, na niwatu ambao huchemka akili zao wanapopata matatizo na hii huwaletea matatizo ya kupata ugonjwa wa kichwa, kuwaza sana, na kuwaletea ugomvi na ndugu zao wakubwa au wakike wenye uso wa duara na maziwa yaliyo tokeza.
Watu hawa hufanya kazi zenye asili ya moto au kudhibiti kama vyuma, magari, wanajeshi, walimu, na kazi zote zenye kuhusu akili nyingi na maamuzi.
Watu hawa wanashauriwa wasijiingize kwenye maswala ya kisiasa na ushindani ushindani wa kimaneno na kimadaraka kwani huzimwa na watu wenye asili ya maji, watu hawa hutumia nguvu nyingi katika utafutaji wa pesa kwani wanapokosa pesa huwe ni wenye huzuni sana na ni watu wenye kujikweza wanapopata pesa na ni watu wenye kupenda kuwakosoa wenzao pasipo wao kukosolewa, watu hawa ni wenye bahati ya kupata wapenzi wenye umaarufu, usomi, utafutaji.
Ila wanawake wenye asili hiii ya moto huwa ni watafutaji na washindani na wenza wao au marafiki zao na huwa wanapata na huwa hawakubali kushindwa hili pia ni hatari kwao kinyota kwani mwisho wao hupata maradhi yatokanayo na damu na watu hawa wapenzi wao ni watu wenye asili ya upepo.
Watu hawa maadui wao wengi ni watu wenye asili ya maji na utafutaji wao na maradhi yao huwa ni yenye asili ya udongo ndio maana huchoka sana baada ya shughuli zao na maungo yao kuuma kuanzia kichwani, mgongoni, mbavuni, mabegani.
Madini yao ni madini yenye aasili ya moto mfano chuma, bati na dhahabu na vito vyao vingi vyenye asili ya wekundu rangi ya moto, rangi ya safaya na rangi ya orange na wanashauriwa kwenye majumba yao au vitu vyao wapakae rangi zinazofanana na hizo na sadaka zao nyingi ziwe zina asili ya kuchinja hasa wanyama wenye asili ya wekundu madume na kahawia madume na nyota zao ni nyota za punda, simba na mshale, siku zao nzuri huwa ni jumanne, alhamisi na jumapili, vyakula vyao viwe ni vyakula visivyo ondolewa kiiini wajiepushe kula vyakula visivyokuwa na radha na mafusho yao ni kisti, sandarusi na udi uliochanganywa na kafru wapende dawa zenye asili ya kuchomwa zitawasaidia sana wasipende kuishi karibu na maji au sehemu yenye machimbo machimbo hayo ni maelezo kwa ufupi tu.
 Watu wenye asili ya hii kwa mwaka huu
Watu wenye asili hiii ya moto kwa mwaka huuu wamejikuta wakiahangaika sana katika utafutaji wa mali na kazi pasipo faida yoyote na wapenzi wao wamejikuta katika hali ngumu ya kimaisha na wamejikuta maadui zao ni wale wanawake wanaoshirikiana na mabosi zao kwahiyo wana uzito katika maswala yao wanashauriwa wasikate tamaa kwani mwaka unaokuja ni wafaraja kwao, mambo yao yatakuwa yana nafuu kwanzia mwezi wa sita mpaka wasaba au watakapotembelewa na mtu mwenye uso wa duara na mwenye misuli na mwenye kutumia vitu vyenye asili ya moto moto na watu wenye asili hiii hasa wanaume wako kwenye hali ngumu ya kimaisha kwa sasa, anapigishana kelele na mpenzi wake mwenye asili ya kuongeongea sana na watu hawa wamekutwa na matatizo ya msiba au ugonjwa kwa watu wa karibu wao kwa mwaka huu wa 2011 na mpaka sasa hawajapata suruhisho la matatizo yao na walipo sasa wanatafuta msaada kwa watu wa karibu wao pasipo mafanikio makubwa.
Watu wenye asili hii kwa mwaka 2012
Ni mwaka wa faraja kwao haswa unapofika katikati ya mwaka huo na wanashauriwa waende safari zao kwa upande wa mashariki na waondoke wakati wa mvua kuisha na wasikimbilie sehemu zenye mvua nyingi hawatafanikiwa wachanganyikane na watu wengi watapata msaada ni wakati mzuri kutumia malizao watafanikiwa au kuomba msaada kwa watoto wao na nchi zenye asili hiii ni wakati mzuri wa kujipanga kwa vita kwani watashinda,
Na tunatabiri 2012 nchi za mashariki zitaendelea kupata milipuko na jua kuwa kali na kutasikika habari za matajiri au watoto wa wakubwa kuchukua madaraka au makaimu wa viongozi wa sasa kuchukua madaraka au vyama vyenye asili ya jina linaloanzia na herufi O au zenye mgombea mwenye uso wa duara au mwenye nywele nyekundu au mwenye kipara katikati ndio watakao chukua uongozi, baadhi ya nchi zitajipanga kijeshi na zitatishia uvamizi na kutakuwa na visasi vya kifamilia, kinchi, kikabila na kidini, Kutakuwa na mkutano wa baadhi ya nchi kutaka kujitenga na kuanzisha majeshi yao na ajali nyingi zitakuwa za mlipuko kwa nchi za mashariki, mvua zitakuwepo na kutakokea mafuriko katika nchi zenye wanyonge wanyonge.





1 comment: